ONYO - Maafisa wa Urusi wanaeneza uongo kuhusu uvamizi kamili wa Putin wa Februari 2022 nchini Ukraine. Ujumbe unaofadhiliwa na serikali kwenye mitandao ya kijamii na programu za kutuma ujumbe unaionyesha Urusi kuwa nchi  karimu katika masuala ya kibinadamu inayotatua mateso yaliyosababishwa na serikali ya Ukraine.
UONGO
UKWELI
UONGO
UKWELI

1/9

“Kwa miaka minane iliyopita, Urusi imekuwa ikilinda maisha na afya ya raia nchini Ukraine.”

Kuanzia uvamizi wake wa kwanza nchini Ukraine mwaka 2014 hadi uvamizi wake kamili mwaka wa 2022, Urusi ilitengeneza janga la kibinadamu ambalo inadai kuwa inaliondoa.

Kabla ya uvamizi kamili wa Februari 24, 2022, uvamizi wa miaka minane wa Urusi mashariki mwa Ukraine ulisababisha vifo vya watu 14,000 na wengine zaidi ya  milioni 1.4 kusajiliwa  kuwa wakimbizi wa ndani, kwa mujibu wa  Umoja wa Mataifa. Tangu Kremlin ilipoivamia zaidi Ukraine mwaka 2022, mashambulizi ya mabomu na ukatili wa vikosi vya Urusi  ulisababisha raia milioni 6.5 wa Ukraine kukimbia  makwao ili kutafuta hifadhi katika nchi jirani na mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi wa ndani.

FICHUA UONGO. SHIRIKI UKWELI.

Shuka Chini
╲╱

Wanawake wa Ukraine wakikusanyika katika umati.
Wanawake wa Ukraine wakikusanyika katika umati.

Wananchi wa Ukraine wanasubiri usambazaji wa chakula ulioandaliwa na Shirika la Msalaba Mwekundu huko Bucha, viungani mwa Kyiv, Jumatatu, Aprili 18, 2022. (© Emilio Morenatti/AP Photo)

UONGO
UKWELI
UKWELI
UKWELI

2/9

“Vikosi vya siasa vya mrengo wa kulia vya Ukraine vilivyoingia madarakani kwa njia zisizo za kikatiba mwaka wa 2014 vimechukua hatua za kijeshi dhidi ya wakaazi wa mikoa inayozungumza Kirusi nchini humo ambao wanakataa kutambua uhalali wa serikali.”

Hakuna vikosi vya siasa vya mrengo wa kulia vilivyoingia madarakani nchini Ukraine mwaka wa 2014.

Wazungumzaji wa Kirusi nchini Ukraine wanaweza kutumia kwa uhuru haki zao za kibinadamu uhuru wa kujieleza, kukusanyika kwa amani, na kujumuika tofauti na raia wa Urusi chini ya utawala wa kiimla na ukandamizaji wa Putin. Operesheni ya Putin inayoitwa "operesheni maalum" ya "kukomboa" wazungumzaji wa Kirusi nchini Ukraine imeua maelfu ya raia katika miji yenye watu wengi wanaozungumza Kirusi kama vile Kharkiv, Kherson, na Mykolayiv, bila kusahau Mariupol na eneo la Donbas.

“Revolution of Dignity“ (Mapinduzi ya Kurejesha Utu) ya Ukraine mwaka wa 2014 yalikuwa vuguvugu maarufu la kidemokrasia lililojitokeza mitaani kuunga mkono ushirikiano kamili wa Ukraine na Ulaya. Baada ya msako mkali ulioua zaidi ya waandamanaji 100 wa amani, Rais wa wakati huo Yanukovych aliyeungwa mkono na Kremlin alitoroka nchini na kuelekea Urusi. Serikali ya mpito iliyoundwa haraka ilipanga uchaguzi wa rais mwezi Mei 2014 na uchaguzi wa wabunge Oktoba 2014.

Chama cha siasa kali za mrengo wa kulia “The Right Sector“ kilishindwa kupata asilimia 5 ya kura zilizohitajika kuingia Bungeni na hakikuwa sehemu ya serikali mpya.

FICHUA UONGO. SHIRIKI UKWELI.

Shuka Chini
╲╱

Mwanamke akiwa amesimama mbele ya mstari wa kupiga kura akiwa ameshika karatasi ndefu.
Mwanamke akiwa amesimama mbele ya mstari wa kupiga kura akiwa ameshika karatasi ndefu.

Raia wa Ukraine wakiwa kwenye foleni kupokea kura zao katika kituo cha kupigia kura wakati wa uchaguzi wa urais na meya mjini Kyiv, Ukraine, Jumapili, Mei 25, 2014 (© Sergei Chuzavkov/AP Photo)

UONGO
UKWELI
UONGO
UKWELI

3/9

“Makubaliano ya Minsk ni uthibitisho kwamba jumuiya ya kimataifa ilitambua unyanyasaji katika sehemu ya watu wanaozungumza Kirusi kati ya idadi ya watu wa Ukraine na jukumu la Ukraine katika kuunda mgogoro wa jumla wa kibinadamu.” 

Shirikisho la Urusi — sio Ukraine — lilianzisha vita katika mkoa wa Donbas mashariki mwa Ukraine.

Mnamo Aprili 2014, Shirikisho la Urusi lilituma vikosi maalum vya operesheni huko Donetsk na Luhansk kuchukua udhibiti wa eneo hilo na kuanzisha majimbo vibaraka (proxy statelets). Kisha ikafuatwa na vikosi vya kawaida vya jeshi kutoka Urusi. Mapigano hayo yaliyochochewa na Urusi yalisababisha juhudi za kidiplomasia za kuanzisha usitishaji mapigano kupitia mikataba ya Minsk. Urusi ilikiuka mara kwa mara ahadi zake chini ya makubaliano ya Minsk na kuendelea kuendeleza mzozo mbaya wa miaka minane mashariki mwa Ukraine, na kusababisha mateso yasiyoelezeka kwa idadi kubwa ya watu wanaozungumza Kirusi ambayo ilikuwa inadaia kuwalinda.

FICHUA UONGO. SHIRIKI UKWELI.

Shuka Chini
╲╱

Mwanamke mwenye madoa ya damu usoni akitazama kwa mbali.
Mwanamke mwenye madoa ya damu usoni akitazama kwa mbali.

Natalia Rudneva, 59, aliyejeruhiwa, akionyesha hisia mwanawe alipokuwa analazwa hospitalini baada ya shambulio la risasi usiku huko Kramatorsk, Ukraine, Alhamisi, Mei 5, 2022. (© Andriy Andriyenko/AP Photo)

UONGO
UKWELI
UONGO
UKWELI

4/9

“Licha ya makubaliano ya Minsk, katika kipindi cha miaka minane iliyopita, serikali ya Ukraine imezingira Donbas, kushambulia kwa makombora makazi ya raia na kuharibu miundombinu ya matibabu na kiraia.” 

Urusi yenyewe ndiyo ya kulaumiwa kwa vifo na uharibifu.

Donbas ni eneo la Ukraine ambalo Urusi ililivamia na kwamba wawakilishi wa Kremlin wanalidhibiti kwa nguvu. Ukraine haivamii Donbas. Ukraine inalinda na kupigania kurejesha eneo lake, lililovamiwa na Urusi na wawakilishi wake.

Urusi na wawakilishi wake walichukua udhibiti wa sehemu za Donbas na kwa kufanya hivyo ilichukua jukumu la kimaadili la kuwapa watu katika eneo hilo huduma, huku ikizuia serikali ya Ukraine kufanya hivyo katika maeneo ambayo haikudhibiti.

Serikali ya Ukraine ilianzisha kliniki, ikijumuisha vituo vya chanjo ya COVID-19, kando ya mstari wa mawasiliano kati ya vikosi vya Ukraine na vile vya Urusi na wawakilishi wake, na raia wa Ukraine wanaoishi katika maeneo yanayodhibitiwa na Urusi walilazimika kuvuka vituo vya ukaguzi ili kupata huduma hizo na kutembelea familia. Kuanzia Machi 2020, wawakilishi wa Urusi walitumia COVID-19 kama kisingizio cha kufunga vituo vya ukaguzi, na kuwazuia zaidi raia wa Ukraine kusafiri kwa uhuru ndani ya nchi yao.

FICHUA UONGO. SHIRIKI UKWELI.

Shuka Chini
╲╱

Mwanamume aliyejifunga bandeji yenye damu kichwani akiwa ameketi kwenye kochi dogo huku akiushika uso wake mikononi.
Mwanamume aliyejifunga bandeji yenye damu kichwani akiwa ameketi kwenye kochi dogo huku akiushika uso wake mikononi.

Mkazi wa eneo hilo aliyejeruhiwa katika shambulio la bomu lililofanywa na vikosi vya Urusi amepumzika katika hospitali ya Pokrovsk, mashariki mwa Ukraine, Jumatano, Mei 25, 2022. Makombora mawili yalishambulia mji huo mapema asubuhi, na kusababisha majeruhi wasiopungua wanne. (© Francisco Seco/AP Photo)

UONGO
UKWELI
UONGO
UKWELI

5/9

“Maafa haya makubwa ya kibinadamu yalipoongezeka, Urusi iliingilia kati kutoa msaada kwa watu walioathiriwa katika mikoa ya Donetsk na Luhansk ya Ukraine, kupeleka dawa, vifaa vya matibabu na matibabu."”

Vita vya uchokozi vya Urusi vilisababisha janga hili la kibinadamu.

Serikali ya Urusi pekee ndiyo inahusika katika kuzorota kwa hali ya kibinadamu. Kwa uvamizi wake zaidi nchini Ukraine mnamo 2022, Urusi iliongeza kwa njia kubwa janga la kibinadamu.

Serikali ya Urusi ilichochea mzozo mashariki mwa Ukraine mnamo 2014 kwa kutumia huduma zake za kijasusi na washirika wanaoungwa mkono na Kremlin. Tangu wakati huo, Kremlin imetumia kwa kejeli suala la misaada ya kibinadamu kuendeleza propaganda.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari, katika muda wa miaka minane tangu uvamizi wake wa kwanza mwaka 2014, Urusi ilijaribu kuficha usafirishaji wake wa silaha na zana za kijeshi kutoka Urusi kuvuka mpaka hadi mashariki mwa Ukraine, ikidai misafara hiyo ilikuwa ikipeleka "msaada wa kibinadamu" nchini Ukraine. Wakati wa vita vyake vya sasa visivyo na msingi dhidi ya Ukraine, vikosi vya Urusi viliripotiwa kuvamia misafara halisi ya kibinadamu. Urusi ilianzisha maafa ya kibinadamu kusini-mashariki mwa Ukraine na kudhibiti eneo hilo, na hivyo kufanya Ukraine isiweze kutoa huduma za matibabu kama vile usafiri wa ndege ya wagonjwa katika eneo ambalo Ukraine haidhibiti.

FICHUA UONGO. SHIRIKI UKWELI.

Shuka Chini
╲╱

Mwanamume akiwa amembeba msichana mdogo mwenye miguu iliyofungwa bendeji kwenye barabara ya ukumbi.
Mwanamume akiwa amembeba msichana mdogo mwenye miguu iliyofungwa bendeji kwenye barabara ya ukumbi.

Yana Stepanenko, 11, amebebwa na daktari katika hospitali ya umma huko Lviv, Ukraine, Ijumaa, Mei 13, 2022. Yana na mama yake, Natasha, 43, walijeruhiwa Aprili 8 wakati wa shambulio la makombora la Urusi kwenye kituo cha gari-moshi cha jiji la mashariki ya Kramatorsk, ambako walisafiri kutoka kijiji chao karibu na mstari wa mbele. Walikuwa wakipanga kupanda treni ya uokoaji iliyokuwa ikielekea magharibi na, walitumaini, kuelekea maeneo salama. (© Emilio Morenatti/AP Photo)

UONGO
UKWELI
UONGO
UKWELI

6/9

“Mnamo Februari 2022, mambo yaliharibika zaidi wakati Dmytro Kuleba, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, alipomwarifu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwamba makubaliano ya Minsk hayatatekelezwa ‘kwa masharti ya Urusi.’”

Urusi haina nia ya kuheshimu makubaliano yake au kusuluhisha mzozo.

Urusi ilikosa kutekeleza makubaliano ya Minsk - sio Ukraine. Kuanzia 2014, Ukraine ilichukua hatua za kutekeleza makubaliano ya Minsk. Ilikuwa ni Urusi ambayo ilikosa kutekeleza usitishaji mapigano na kuondoa vikosi vyake, kama ilivyohitajika.

FICHUA UONGO. SHIRIKI UKWELI.

Shuka Chini
╲╱

Mwanamke amesimama mbele ya rundo kubwa la kifusi.
Mwanamke amesimama mbele ya rundo kubwa la kifusi.

Anna Shevchenko, 35, anaonyesha hisia akiwa karibu na nyumba yake huko Irpin, karibu na Kyiv, Jumanne, Mei 3, 2022. Nyumba hiyo, iliyojengwa na babu na nyanya ya Shevchenko, iliharibiwa na mlipuko wa bomu ya Urusi mwishoni mwa Machi wakati wa uvamizi wake kamili nchini Ukraine. (© Emilio Morenatti/AP Photo)

UONGO
UKWELI
UONGO
UKWELI

7/9

“Baada ya Ukraine kuashiria kuwa haitazingatia makubaliano ya Minsk, ilianza kupeleka vikosi vyenye silaha na kutishia maisha ya zaidi ya raia milioni nne katika eneo hilo. Lengo? Ili kuunda hali za kuondoa idadi ya watu katika maeneo yanayozungumza Kirusi nchini Ukraine.”

Wataalamu wa Unazi (Nazism) na Vita vya Dunia vya pili walionyesha upinzani wao mkubwa kwa jaribio la Putin la kulinganisha Ukraine na serikali yake iliyochaguliwa kidemokrasia na ile ya Ujerumani ya Nazi.

Kikundi cha wanahistoria mashuhuri na wasomi walitia sahihi barua iliyoshutumu serikali ya Urusi “kwa matumizi mabaya ya kijinga ya neno mauaji ya halaiki (mauaji ya kimbari) (Genocide), kumbukumbu ya Vita vya Pili vya Dunia na Mauaji makubwa (Holocaust), na kulinganisha serikali ya Ukraine na utawala wa Nazi ili kuhalalisha uuvamizi wake usio na msingi.”

FICHUA UONGO. SHIRIKI UKWELI.

Shuka Chini
╲╱

Msururu wa mifuko ya miili iliyotandazwa chini huku umati wa wanaume ukiizunguka.
Msururu wa mifuko ya miili iliyotandazwa chini huku umati wa wanaume ukiizunguka.

Kaburi la pamoja lafukuliwa na mamlaka za eneo hilo mnamo Aprili 8, 2022, wanapojaribu kutambua miili ya raia walioangamia wakati ambapo majeshi ya Urusi yalikuwa yakidhibiti Bucha, Ukraine. (© Andalou Agency/Getty Images)

UONGO
UKWELI
UONGO
UKWELI

8/9

“Na wakati Warusi wanatoa huduma na matibabu kwa wanajeshi wa Ukraine waliojeruhiwa, Vikosi vya Wanajeshi vya Ukraine vinaharibu miundombinu ya matibabu. Wamegeuza taasisi za matibabu kuwa ghala za kijeshi na wamefikia hatua ya kushambulia ambulensi na wafanyikazi wa matibabu.”

“Hata wanaiba na kuuza tena misaada ya kibinadamu.” 

Wakati wa vita vyake visivyo na msingi dhidi ya Ukraine, vikosi vya Urusi viliripotiwa kuvamia misafara ya kibinadamu.

Kuna simu zilizonaswa na ripoti nyingi za wanajeshi wa Urusi wakipora nyumba nchini Ukraine, wakichukua vifaa vya kawaida vya nyumbani kuanzia kwa mashine ya kufulia hadi rangi ya kucha na kuvisafirisha kupitia Belarus kwa familia zao nchini Urusi.

FICHUA UONGO. SHIRIKI UKWELI.

Shuka Chini
╲╱

Mkono ulioshika simu ya mkononi inayoonyesha picha.
Mkono ulioshika simu ya mkononi inayoonyesha picha.

Imenaswa kwenye simu ya mkono, kamera ya kuhifadhi video ya duka inaonyesha mwanajeshi wa Urusi akiwa amevalia tu koti lake la kuzuia risasi, bunduki, balaclava, flip-flops na chupi, akipora duka lililoharibiwa ambapo picha ilipigwa Aprili 22, 2022, huko. Trostyanets, Ukraine. (© Gaelle Girbes/Getty Images)

UKWELI
UKWELI
UKWELI
UKWELI

9/9

“Mashirika ya kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa na Shirika la Afya Duniani yanapaswa kufanya jambo fulani kuhusu Ukraine kupuuza kabisa sheria ya kibinadamu, uharibifu wa vituo vya afya, na unyanyasaji wao wa kinyama kwa raia na wanajeshi wa Urusi.” 

Mwaka wa 2014, Urusi iliiteka Crimea kwa nguvu na kuanzisha mzozo mashariki mwa Ukraine. Leo, Urusi inapigana vita kamili bila sababu na isiyo ya haki dhidi ya Ukraine.

Miongoni mwa mashambulizi mengine ya mabomu, Urusi ilitumia mabomu yenye vilipuzi na vipande vya chuma vinavyotawanyika, kupiga vituo vya huduma ya afya na miundo msingi mingine ya kiraia, na kugeuza jiji la Mariupol kuwa eneo la maafa yasiyoweza kuepukika.

Marekani imetathmini kuwa wanajeshi wa Urusi wamefanya uhalifu wa kivita nchini Ukraine. Habari kutoka kwa idadi inayoongezeka ya miji inaonyesha ushahidi zaidi wa ukatili wa vikosi vya Urusi.

FICHUA UONGO. SHIRIKI UKWELI.

Shuka Chini
╲╱

Wanaume wawili waliovalia nguo za kiraia wakiwa wamekufa kwenye ua.
Wanaume wawili waliovalia nguo za kiraia wakiwa wamekufa kwenye ua.

Miili ya wanaume walioripotiwa kuuawa na wanajeshi wa Urusi imelala kwenye uwanja mnamo Aprili 5, 2022, huko Bucha, Ukraine. Mamia ya miili imepatikana katika siku chache tangu vikosi vya Ukraine kudhibiti tena mji huo. (© Oleg Pereverzev/Global Images Ukraine/Getty Images)